VICHWA VIPYA KWENYE ‘GRAPHICS' & 'EDITING' BONGO!!
 |
..Frank na Francis |
 |
wakishoo love na swagga na baba yao katikati... |
 |
Mapacha wakiwa moja ya kazi yao walio idizaini.. |
Vichwa vipya kwenye ‘graphics’ na ‘editing’ ya filamu Bongo
KONA ni Msanii wa Jahazi inayotoka kila Jumapili. Awali ya yote natumaini huu mzima wa afya ungana nami leo utapata kujua mengi kutoka kwa vijana wenye umri mdogo kwenye tasnia hii ambao wamebobea kwenye masuala ya usanifu ‘graphics’ na kuhariri ‘editing’ katika filamu, muziki na picha na pia ni watayarishaji na wandaaji wa filamu, muziki na vipindi mbalimbali vya tv na redio katika anga ya Tanzania.
Hao si wengine ni Frank na Francis ‘The Squares’ ama ‘Swagger-Rockerz Anthem’ ambao ni mapacha na kwa hali halisi ata ukiwaona kwa harakaharaka utashangazwa na uwezo wao huo wawapo kwenye kazi yao ya graphics pamoja na ya uongozaji ‘director’.
Frank na Francis ni watoto wa pili kwa baba yao, George Ntevi, walizaliwa Mei 30, 1992, ambapo elimu yao ya msingi walisomea shule ya msingi Muhimbili 1999-2005, baada ya hapo walifanikiwa kusoma elimu ya sekondari, kwenye Shule ya Magomeni Sekondari ambayo awali ilikuwa ikijulikana kama Green Acres Magomeni.
Walifanikiwa kuchaguliwa shule ya sekondari ya Tambaza wote kwa pamoja na kwa sasa wapo kidato cha sita.
 |
Mapacha wakisho love.. Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo: Mwandishi: Kwanza nawapongeza kwa kazi zenu nzuri.
Mapacha: Asante, nasi tunashukuru. Mwandishi: Nilikuwa nataka kufahamu mengi zaidi juu ya kipaji chenu katika masuala ya graphics na uandaaji wa filamu, isitoshe kwa umri wenu ni nadra sana kwenye anga hizi!
Mapacha: Ok, kwanza tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uwezo huu mkubwa tulionao, nasi tunafarijika sana ila nyuma yetu baba yetu mzazi na watu baki ni msaada tosha kufikia malengo haya, ni hakika huu ni mwanzo tu ila tuna ndoto ya kufanya makubwa zaidi ya hapa.
Mwandishi: Masuala haya yote mulianza lini na mlipatia wapi ujuzi huu!
Mapacha: Ni hakika bado tutaendelea kumshukuru Mungu ila, ni utundu wetu ndio uliosaidia kujua haya yote.
“Awali tulipokuwa na miaka 12, baba alikuwa akituachia kompyuta, ambapo kwa kujaribu kuchezea tukajikuta tunafanya baadhi ya vitu ambavyo vilionekana kutuvutia hasa wakati huo tulikuwa tunatumia programu ya ‘Window Move Maker”.
Pia tuliweza kutumia programu za Adobe after effect na 3D, ni hakika tulitumia akili nyingi kujifunza programu hizi hasa kutokana na ugumu wake na kwa msaada mkubwa tuliweza kupata walimu waliotusaidia, wakiwemo Green Malwa wa TBC na Jacob Ubwe, ambaye alikuwa mtaalamu mstaafu wa Kampuni ya simu ya TTCL.
Mwandishi: Kwa kawaida programu hizi za 3D na adobe after effect huwa zinaumiza kichwa wataalamu wengi, kwenu nyie ilikuwaje?
Mapacha: Kwetu ilikuwa ngumu ila kwa kuwa tulikuwa na nia ya kujua tulifanya juu chini ili kufanikisha lengo letu.
“Baba alipoona tumefikia malengo na kubobea katika masuala ya graphics na utayarishaji wa kazi za video, kwa kuona umuhimu wetu aliweza kununua kompyuta ya Marc Pro interl Xeon ambayo ni maalumu katika masuala haya,” anasema Frank. Mwandishi: Mpaka sasa mmeshafanya kazi ngapi katika masuala haya haya ya graphics na uandaaji?
Mapacha: Kazi tulizofanya ni nyingi sana, tunamshukuru baba yetu kwa yote kwani kwa kupitia studio yake ya Ntevi Pro Vision ya Magomeni jijini Dar es Salaam, tumeweza kutengeneza na kudizaini logo mbalimbali kwa kutumia graphics zilizo na ubora na pia kazi nyingi za ma-director wakubwa wamekuwa wakituletea kutia mkono wetu hivyo mara nyingi katika mambo haya huwa kuna siri kubwa, hivyo hatutaweza kuzitaja baadhi ya kazi hizo.
Sambamba na hilo pia tumeweza kufanya filamu ya ‘The Magic Flower’ ambayo tuliiongoza sisi wenyewe pamoja na graphics, ni hakika filamu hii itakuwa kali zaidi kati ya filamu zote za kibongo, kwani imejaa ubora wa hali ya juu,” anasema Francis.
Mwandishi: Nini siri ya kujiita majina ya ‘The Squares’ na ‘Swagger-Rockerz Anthem’?
Mapacha: Jina ili lilikuwa linatutambulisha kwa kuwa herufi zetu za mwanzo zinaanzia na F, hivyo kipindi kundi la The Square la Nigeria lilipokuwa likitamba, wengi tuliokuwa tukisoma nao sekondari walikuwa wakitufananisha na kundi hilo, hivyo jina hili liliweza kutamba hakika mpaka leo hii na hili la Swagger Rockerz Anthem, ni jina ambalo tunalitumia sana kwa sasa Tambaza High School.
Mwandishi: Munatoa maoni gani juu ya ma-graphics na ma-director wazoefu hapa Tanzania?
Mapacha: Aaaah! Ok, kwa sasa bado tupo shule, zaidi tunataka kupiga kitabu mpaka ngazi ya chuo kikuu, na baada ya hapo tunaingia rasmi, hivyo wakongwe wajue kuna vichwa na damu changa katika masuala haya ya ‘editing na graphics’, zaidi pia wakasome ili kuleta changamoto.
Kuchanganya picha iwe ya filamu ama muziki kwa sasa teknolojia zinakua na kuna mabadiliko kibao zaidi, kunahitajika umakini mkubwa hivyo bila kusomea ni kazi bure, zaidi maproducer wakisoma nadhani kazi na sanaa za Tanzania zitakuwa na soko kubwa.
Mwandishi: Mna ujumbe gani kwa vijana wenzenu kwa sasa walioko mitaani?
Mapacha: Zaidi wajaribu kuwa wabunifu na wasikae vijiweni, wajaribu hata kusomea vyuo vidogo vidogo vilivyopo hapa nchini kwani vijiwe haviongezi tija yoyote zaidi ya kuzalisha maovu.
Francis na Frank wanaishi Magomeni, jijini Dar es Salaam, na wanafanya kazi hizo chini ya Studio ya Ntevi Pro Vision, ambayo ni ya baba yao, George Ntevi, ambaye naye ni mkongwe katika masuala hayo, ikiwamo ya kupiga picha za mnato na ‘video shooting’ kwenye sherehe na hafla mbalimbali hapa nchini. kwa mawasiliano zaidi +255719076376 ama chale family@yahoo.com |